Yacine Brahimi amefanikiwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika BBC mwaka huu na kufanikiwa kuwa mualgeria wa kwanza kutwaa tuzo hiyo tangu miaka 23 ya historia ya tuzo hiyo.
Mchezaji huyo aliyezaliwa ufaransa ni moja ya nyota wenye uwezo mkubwa wa kucheza katika nafasi ya kiungo mshambuliaji na kiungo wa pembeni.
Ameshukuru watu walioweza kumpigia kura na kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo ambayo ameitoa zawadi kwa Algeria na kwa Afrika kwa ujumla.
Brahim aliingiza bao la ushindi dhidi ya mabingwa wa Hispania Barcelona, bao lengine la kisasa katika ligi ya mabingwa wa ulaya na kisha kuwa katika msitari wa mbele wakati nchi yake iliposonga mbele katika michuano ya kombe la dunia
Aliwapiku wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast na hatimaye Yaya Toure - aliyenyakua ushindi mwaka jana.
Washindi waliopita wa tuzo za bbc afrika
2013: Yaya Toure (Manchester City & Ivory Coast)
2012: Chris Katongo (Henan Construction & Zambia)
2011: Andre Ayew (Marseille & Ghana)
2010: Asamoah Gyan (Sunderland &
Ghana)
2009: Didier Drogba (Chelsea & Ivory Coast)
2008: Mohamed
Aboutrika (Al Ahly
& Egypt)
2007: Emmanuel
Adebayor (Arsenal
& Togo)
2006: Michael Essien (Chelsea & Ghana)
2005: Mohamed Barakat (Al Ahly & Egypt)
2004: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2003: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2002: El Hadji Diouf (Liverpool &
Senegal)
2001: Sammy Kuffour (Bayern Munich & Ghana)
2000: Patrick Mboma (Parma & Cameroon)
0 comments:
Post a Comment