Home » » SAIMON MSUVA ANAPOGONGANISHA VICHWA VYA YANGA, AANZE KIKOSI CHA KWANZA AU ATOKEE BENCHI?

SAIMON MSUVA ANAPOGONGANISHA VICHWA VYA YANGA, AANZE KIKOSI CHA KWANZA AU ATOKEE BENCHI?

Saimon Msuva alitokea benchi na kuifungia timu yake mabao mawili katika mchezo wa ligi kuu tanzania bara kati ya yanga sc na jkt mgambo. msuva aliingia uwanjani dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima alifunga bao la kwanza katika dakika 73 baada ya kuvunja mtego wa kuotea ambao uliwekwa na wachezaji wa mgambo, akafunga tena katika dakika ya 88 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga.
dakika 28 tangu aichukue nafasi ya Niyonzima, kiungo mshambulizi, msuva alifunga bao kuongoza kwa timu yake. Msuva amewahi kuniambia kuwa anapendelea kucheza katika mfumo wa 4-4-2 kwa madai kuwa ndiyo mfumo uliozoeleka kwa wachezaji wengi wa kitanzania. wakati alipoanza kupewa nafasi katika kikosi cha Yanga na kocha, Ernie Brandts mchezaji huyo alikuwa akiwaboa hadi mashabiki wa klabu yake kutokana na uchezaji wake wa stahili moja tu.
Msuva alitawala nafasi ya wingi, namba-7 lakini alikuwa akicheza huku akitazama chini zaidi. niliwahi kumuuliza kuhusu uchezaji wake huo naye akasema kuwa atabadilika taratibu, nilimuelewa kwa vile ni kijana mwenye kutaka kuwa bora siku hadi siku. wakati, Yanga ilipotwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2012/13, Msuva alishiriki kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mabao. hamis kizza na Didier Kavumbagu walitengenezewa magoli mengi na msuva wakati huo. yanga ilipomsaini, mrisho ngassa ilionekana kama vile nafasi ya msuva imepotea katika kikosi cha kwanza.
Brandts alipendelea kuichezesha timu hiyo katika mfumo wa 4-3-3 ambao awali kabla ya ujio wa ngassa, brandts alikuwa akiwapanga, athumani iddi, frank domayo na niyonzima katika eneo la katikati ya uwanja. msuva, kavumbagu na kizza walikuwa wakipangwa katika safu ya mashambulizi. mfumo huo ulikuwa mgumu mwanzoni huku mashabiki wakiuponda kwa sababu timu ilikuwa ikimiliki sana mpira lakini haikuwa ikifunga mabao mengi. brandts alipoteza michezo miwili tu kati ya 26 aliyokuwa kocha wa yanga katika ligi kuu.
alitumia wachezaji wake wa kiungo na safu ya mashambulizi kuifanya timu yake kuwa ngumu kufungika. yanga walitwaa ubingwa wao wa mwisho wakitegemea mabao ya niyonzima katika michezo muhimu ya mwishoni. chini ya Brandts wachezaji walikuwa huru kufanya chochote uwanjani kutumia maarifa yao binafsi kushinda mechi. ujio wa ngassa ulimfanya msuva kupunguza makosa yake mengi ya kiuchezaji, jambo hilo lilimfanya kuanza kwa makali katika msimu wa 2013/14. alikuwa mpigaji mahiri wa krosi pasi za mwisho. ngassa alipomaliza adhabu yake na kurudi kikosini.
msuva alirudishwa katika benchi. alirudi kwa kasi katika mzunguko wa pili. brandts akamsogeza ngassa katika safu ya ushambuliaji wa kati akicheza nyuma kidogo ya kavumbagu, msuva akarudishwa katika kikosi cha kwanza. 
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/11/MSUVA.jpg
Alicheza vizuri mfululizo na mchezo wa mwisho wa msimu aliifungia timu yake bao la kusawazisha katika mchezo dhidi ya Simba. msuva alipasua kwa kasi na nguvu katikati ya mabeki wa simba na kupiga kiki kali ya karibu akiwa ndani ya eneo la hatari. alijitambulisha kama mfungaji wa ziada katika timu.
hans van Pluijm alimtumia zaidi mchezaji huyo kama silaha ya kuvuruga mipango ya ulinzi ya timu pinzani. michezo ya klabu bingwa afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri ilifanya hofu yote ya mashabiki wa yanga kuhusu kipaji cha msuva kuondoka. ni winga wa kisasa mwenye uchezaji wa kizamani. kwa ulinganisho, ngassa unaweza kumfanisha na said maulid ‘ smg’, na msuva unaweza kumfanisha na Steven Mapunda ‘ Garrincha’. baada ya kufunga mabao matatu msimu huu akitokea benchi, je, kuna ulazima wa msuva kupangwa katika kikosi cha kwanza?
kama ndiyo ni mfumo gani ambao utamfaa?. anachotakiwa kufanya maximo labda ni kukubali kumuweka nje Andrey Coutinho na kumpanga Jerry Tetege sambamba na jaja. ngassa na dilunga waendelee kucheza kama wanavyotumika sasa. Msuva anatakiwa kuendelea kutokea nje kwa sababu ana faida kubwa sana wakati timu inapokuwa imeshindwa kutumia mbinu za mwalimu.
Jaja ameonekana kuthibitiwa sana, lakini si kweli kwamba mchezaji huyo si bora. ni mfungaji mzuri na mtoaji mzuri wa pasi. kitu pekee ni kumuongea wasaidizi kwa maana ya kuubadili mfumo wa timu kutoka n3-5-1-1 na kuwa 4-5-1 huku mchezaji mmoja wa nafasi ya kiungo akicheza kando ya jaja. msuva aendelee kutokea benchi kwa sababu mifumo ya maximo inalazimisha kuwa hivyo, ataendelea kuwa bora hata akitokea benchi kwa manufaa ya timu.

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303