Wakati ligi kuu Tanzania Bara ikiwa katika mapumziko kupisha michuano ya chaleni, mechi za kimataifa za fifa na michuano ya timu zilizo chini ya miaka 20 Uhai Cup, Timu ya Ndanda kutoka Mtwara inasubiri Ripoti ya Benchi la ufundi lililochini ya Kocha Abdul Mingange kwa sasa ili kuweza kuongeza wachezaji kwenye kipindi hiki cha mapumziko ambacho pia hutumiwa kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo
Ndanda sc jana baada ya kupokea kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa maafande wa JKT Ruvu, alisikika mmoja wa viongozi wa juu wa klabu hiyo akiahidi kufanya usajili wa wachezaji kadhaa wakongwe kuweza kuwasaidia vijana walioko hivi sasa
Kiongozi huyo alisikika akisema lazima wasajiliwe wakongwe ndipo timu ya Ndanda Itafanya vizuri vinginevyo itashuka daraja
"hapa tunatakiwa kuwaleta wakonggwe wawasaidie vijana wetu hilo halina mjadala kwa kuwa mechi nyingi tunapoteza kwa kukosa wazoefu kwenye timu yetu" alisema kiongozi huyo
Ingawa wachezaji hao hakuweza kuwataja lakini uchunguzi wa Mtandao huu umebaini huenda mmoja wao akawa mzawa wa Mkoa wa Mtwara ambae kwa sasa anaichezea Yanga Afrika Nizar Khalfan
Lakini Uongozi wa Ndanda kupitia Afisa habari wake Idrisa bandali umekanusha taarifa hizo ukisisitiza kuisubiri ripoti ya Kocha Mkuu Abdul Mingange
"hatuwezi kusema chochote kwa sasa kwa kuwa mechi yetu tumemaliza jana na sasa tunasubiri ripoti ya mwalimu tujue nani anaondoka na nani anabaki lakini kuhusiana na hili suala la Nizar mimi nakusikia wewe mwandishi , sijuwi umelitoa wapi wakati ripoti ya kocha haijafika mezani kwetu" alisema Bandali
0 comments:
Post a Comment