Home » » ULIIPATA TAARIFA KUHUSU UPASUAJI ALIOFANYIWA RAIS KIKWETE HUKO MAREKANI? IKO HAPA

ULIIPATA TAARIFA KUHUSU UPASUAJI ALIOFANYIWA RAIS KIKWETE HUKO MAREKANI? IKO HAPA

 
 Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.

Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja unusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.

Taarifa hiyo inasema hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303