Tanzania leo wanaikaribisha Malawi katika mchezo wa kwanza wa
kuwania kupangwa kwenye makundi ya kugombea tiketi ya kucheza Fainali za Kombe
la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Taifa Stars
inakutana na Malawi leo, ikitoka kucheza mechi 11 bila kushinda. Mara ya mwisho
Taifa Stars ilishinda 4-1 dhidi ya Benin Oktoba 12, mwaka jana Dar es Salaam na
tangu hapo imekuwa ikichezea vichapo mfulilizo na kutoa sare.
Stars inacheza na
Malawi siku moja baada ya kocha Mzalendo, Charles Boniface Mkwasa kusaini
Mkataba wa mwaka mmoja na nusu, akirithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amesema jana kwamba Mkwasa amesaini Mkataba wa kudumu Taifa Stars, sawa na wa
mtangulizi wake, Mholanzi Mart Nooij.

Malinzi alimteua
Mkwasa kukaimu Ukocha Mkuu Taifa Stars kwa miezi mitatu tangu Julai na akasema
kwa kuanzia atakuwa anachukua mshahara alikuwa analipwa Nooij.
Nooij aliyekuwa
analipwa dola za Kimarekani 12,500 (zaidi ya Sh. Milioni 25) kwa mwezi,
alifukuzwa mwishoni mwa Juni baada ya Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Uganda
Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mechi ya kufuzu CHAN.
Mkwasa aliwateua
Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ kuwa Mshauri wa Ufundi, Hemed
Morocco kuwa Kocha Msaidizi na Manyika Peter kuwa kocha wa makipa wakichukua
nafasi za Salum Mayanga na Patrick Mwangata.
Aidha, Omar Kapilima
aliteuliwa kuwa Meneja na Hussein Swedi ‘Gaga’ kuwa mtunza vifaa vya timu-
kukamilisha sura mpya kabisa ya benchi la Ufundi la Taifa Stars.
Na tangu hapo timu imecheza mechi tatu bila ushindi ikitoa
sare ya 1-1 na Uganda mjini Kampala kufuzu CHAN, ikifungwa 2-1 na Libya mchezo
wa kirafiki mjini Kartepe, Uturuki na kutoa sare ya 0-0 na Nigeria.
Hayo yalikuwa
mabadiliko makubwa kutoka kwenye timu kufungwa mechi tano mfululizo na kwa
ujumla kucheza mechi 11 bila ushindi chini ya Nooij.
Taifa Stars
watasafiri Ijumaa asubuhi kwenda Malawi kurudiana nao Jumapili mjini Blantyire
na mshindi wa jumla ataingia kwenye Raundi ya pili ya kufuzu ambako atamenyana
na Algeria.
Atakayefuzu mtihani
wa Algeria, atakuwa amefanikiwa kupangwa kwenye Kundi la kuwania tiketi ya
kwenda Urusi mwaka 2018.
Wachezaji wote
wanaocheza nje, Mrisho Ngassa wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC wapo kambini.
Watatu hao wamekuja
wakiwa katika kiwango kizuri, Ngassa akitoka kuisaidia klabu yake kufuzu Robo
Fainali ya Kombe la Telkom Knockout na akina Samata na Ulimwengi wakitoka
kuisaidia Mazembe kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kila la heri Taifa
Stars. Mungu ibariki Tanzania. Amin.