Home » » TANZANIA YACHUKUA RASMI UENYEKITI WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

TANZANIA YACHUKUA RASMI UENYEKITI WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki
Waziri Samuel Sitta akizungumza baada ya kupokea Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo 


Tanzania leo imekabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki baada ya Kenya kumaliza muda wake wa kipindi cha mwaka mmoja.
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta na Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo walipokea Uenyekiti huo katika Mkutano wa Baraza wa Mawaziri uliofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC), Jijini Nairobi, Kenya.
Rais wa Tanzania anatarajiwa kupokea Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki siku ya Jumapili katika Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya utakaofanyika pia hapa KICC.

Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo akisoma taarifa ya Kamati ya Makatibu Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Baraza la Mawaziri. Wengine kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera, Waziri Mh. Samuel Sitta na Mwandishi wa Taarifa za Mikutano Mpya kutoka Uganda Bi. Mary Nankabirwa.
Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki
Mwenyekiti anayemaliza muda wake Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Kenya Bi. Phyllis Kandie (katikati) kabla ya kukabidhi uenyekiti kwa Waziri Samuel Sitta wa Tanzania. Kushoto ni Bw. Mugisha Kyamani kutoka Tanzania ambaye alikua ni Mwandishi wa Taarifa za Mikutano kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita
Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akliwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (kulia).
Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki

Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughilikia Miundombinu Dkt. Enos Bukuku walipokutana Jijini Nairobi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki leo. Wengine ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (kulia).

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303