Wananachi wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Wilaya ya Mtwara Vijijini, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kinana akizungumza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Kibaoni, Mtwara Vijijini leo.
Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Katika Kijiji cha Nanguruwe, Wilaya Mtwara Vijijini.
Mnara wa Kumbukumbu ya Mwanajeshi wa Tanzania , Hamad Mzee aliyeuawa na ndege ya kivita ya wareno baada ya kuzitungua ndege mbili za kivita mwaka 1972 katika Kijiji cha Kitaya mpakani mwa Msumbiji na Tanzania wakati wa mapambano ya kuikomboa Msumbiji
Kinana akitoa heshima katika mnara wa kumbukumbu shujaa Hamad Mzee katika Kijiji cha Kitaya, Mtwara Vijijini
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Kitaya
Kinana akihutubia katika mkutano huo.
Kinana akipanda katika moja ya pikipiki 10 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwa makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini katika mkutano wa hadhara wa katika Kata ya Kitaya.
Kinana akimkabidhi kadi ya CCM mmoja wa wanachama wapya wa chama hicho katika mkutano huo.
Kinana akikunjua bendera wakati wa uzinduzi wa Tawi la CCM la Vijana akatika Kijiji cha Nanyamba
Kinana akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nanguruwe kinachotarajiwa kuwa hospitali ya wilaya Mtwara Vijijini
0 comments:
Post a Comment