Home » » KATIBU MKUU FRIENDS RANGERS AWATAKA NDANDA SC NA MBEYA CITY KUCHANGAMKA

KATIBU MKUU FRIENDS RANGERS AWATAKA NDANDA SC NA MBEYA CITY KUCHANGAMKA

FRIENDS

Klabu za Mbeya City na Ndanda FC zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, zimetahadharishwa na uongozi wa Friends Rangers ya Ligi Daraja la Kwanza kwamba wakichelewa tu basi watawakosa wanandinga wao ambao ni mlinda mlango Daud Gabriel pamoja na washambuliaji, Eliuta Mpepo ‘Demba Ba’ na Dismas Cosmas ‘Balotelli’ wanaowawinda.


Mbeya City na Ndanda kwa nyakati tofauti zimetuma maombi ya kuwataka wachezaji hao kwa ajili ya kuwatumia kwenye ligi kuu.
NDANDA
Katibu Mkuu wa Friends, Herry Mzozo, alisema walipokea maombi ya kutakiwa kwa wachezaji wao lakini wanasubiria viongozi wa timu hizo kwenda kumalizana kwani waliwaahidi watafanya hivyo hivi karibuni.


“Tumepokea ofa kutoka Ndanda na Mbeya City kwamba wanawahitaji wachezaji wetu na sisi tumewakubalia kwani huwa hatuna desturi ya kuwazuia kuondoka lakini viongozi wa timu hizo walituambia tusubiri ndani ya wiki hii watakuja kukamilisha huo usajili,” alisema Mzozo.

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303