Home » » BUNGE LASAMBARATIKA, LAGHAIRISHWA TENA LEO MPAKA JIONI SAA KUMI

BUNGE LASAMBARATIKA, LAGHAIRISHWA TENA LEO MPAKA JIONI SAA KUMI



Mzozo mkubwa umesababisha Bunge la Tanzania kuvunjika usiku huu wakati likiendelea na mjadala wa kashfa ya Escrow, baada ya wabunge kushindwa kukubaliana njia sahihi ya kuwawajibisha baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotuhumiwa kuhusika na sakata la wizi wa Zaidi ya fedha za Tanzania shilingi bilioni 300 kutoka Benki Kuu ya nchi hiyo.
kuwa Bunge hilo limeweka rekodi ya kuwa na mjadala wa muda mrefu Zaidi kuliko wakati mwingine wowote. 
Hadi kufikia kuvunjika kwa kikao hicho ilikuwa ni saa 4.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. 
Spika wa Bunge hilo Anne Makinda karibu muda wote wa kikao hicho alijikuta akitoa tahadhari kwa wabunge wake kujilinda na hatua za kuingilia mihimili mingine ya utawala ya Tanzania ambayo ni Mahakama na Serikali. Hatua hiyo kwa namna Fulani iliamsha hisia tofauti kutoka upande wa kambi ya upinzani pamoja na wajumbe wa kamati ya hesabu za Serikali ambao walitishia kutoka nje hadi viongozi wanaodaiwa kulindwa na bunge hilo wawajibike wenyewe. 
Bunge hilo linategemewa kuendelea na kikao chake hapo saa kumi jioni ya leo

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303