Hatimaye Justin Bieber amevuna matunda ya kosa alilofanya la kurusha
mayai 20 kwenye nyumba ya jirani yake bila kuwa na sababu za msingi.
July 9, Justin Bieber akiwakilishwa na wakili wake aliyefahamika kwa
jina la Shawn Holley amehukumiwa kufanya kazi za jamii kwa muda wa siku
tano ikiwa ni pamoja na kusafisha mazingira. Pia anatakiwa kumlipa
jirani yake $80,900 kama fidia ya uharibifu wa nyumba yake.
Mahakama imemtaka Justin Bieber kukaa umbali usiopungua hatua 100 na
jirani yake wala familia ya jirani huyo kwa kipindi cha miaka miwili na
pia ahudhurie program maalum itakayomsaidia kudhibiti hasira (enger
management program).
0 comments:
Post a Comment