KLABU ya waandishi wa habari mkoani hapa imekamilisha hatua muhimu
katika kuanzisha chama cha kuweka na kukopa kwa wanahabari na wadau wao
kitakachojulikana kama Mtwara media saccos.
Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo mipango na uchumi wa klabu ya
waandishi wa habari mkoani Mtwara MTPC. Godwin Msalichuma aliwaambia
waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa hatua iliyofikiwa sasa ni ya
uandikishaji wa wanachama baada ya kumaliza kuipitia rasmu ya katiba ya
chama hicho.
Msalichuma alisema kuwa rasimu ya katiba iliyoandaliwa na kamati
maalumu iliyoundwa kuitunga na kisha kupitiwa na waandishi na wadau wote
na kuweka mapendekezo yao na hatimaye kamati ilikaa tena na kuiboresha
na sasa imekamilika tayari kwa kutumika kama katiba rasmi ya chama
hicho.
“Hatua ya kwanza ilikuwa kuandika katika ambayo iliandikwa na
ilizinduliwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara Wilman Ndile katika mkutano wa
wadau uliofanyika januari mwaka huu…baada ya hapo ilipitiwa na
wanahabari na wadau wao kisha ilirejeshwa kwa kamati ambayo imeipitia na
sasa ipo tayari kwa kutmika”, alisema Msalichuma ambaye pia ni katibu
msaidizi wa klabu hiyo.
Mwenyekiti huyo alisema wanahabari na wadau kadhaa wamejitokeza
kujiandikisha na kujiunga na chama hicho chenye lengo la kuwajengea
uwezo kiuchumi wanahabari mkoani humo ambao wengi wao ni wale ambao
hawana sifa za kupata mikopo kutoka taasisi za fedha kama vile mabenki
na taasisi nyingine.
“Kama mnavyofahamu wanahabari wenzangu lengo la kuanzishwa kwa chama
hiki ni kuhakikisha wanahabari wanapata mikopo itakayowawezesha
kuanzisha miradi ya kiuchumi na kununua vifaa vya kufanyiakazi pamoja na
kujiendeleza kielimu na kusomesha watoto wao…ili litafanikiwa kama
tutajiunga kwa wingi”, alisema Msalichuma.
Msalichuma alisema kuwa chama hicho kitakapokamilika kitakuwa ndio
mkombozi wa kiuchumi kwa wanahabari mkoani humo ambapo kitatoa mikopo
kwa masharti nafuu kwa wanachama wake ili kuwawezesha wote kukopa na
mikopo hiyo itakuwa ni kwaajili ya kujiendeleza kielimu, kuanzisha
miradi ya kiuchumi na kununua vifaa vya kufanyiakazi.
Akizungumzia masharti ya kujiunga mwenyekiti huyo alisema kuwa
wanaoruhusiwa kujiunga ni wanahabari wote wanaoishi na kufanyakazi zao
ndani ya mkoa wa Mtwara bila kujali ni wanachama wa MTPC au hapana,
wafanyakazi wote wanaofanyakazi katika vituo vya redi ambao sio
waandishi wa habari pamoja na wadau wa habari wanaoishi mkoani humu.
Aidha Msalichuma alisema kuwa chama hicho ambacho kwa sasa
kinaendeshwa chini ya uongozi wa juu wa MTPC kinatarajiwa kupata
viongozi wake miezi mitatu ijayo ambapo kitafanya mkutano mkuu wa kwanza
wa uchaguzi na kuwapata viongozi watakaokiongoza kwa miaka mitatu kwa
mujibu wa katiba.
0 comments:
Post a Comment