Shirikisho la soka nchini Nigeria limepigwa stop na shirikisho la soka
duniani FIFA, kufuatia mzozo wa viongozi wa shirikisho hilo dhidi ya
wale wa serikali ya nchi hiyo ya magharibi mwa barani Afrika.
FIFA wamelipiga Stop shirikisho la Nigeria NFF, baada ya maafisa wa
serikali kutangaza amri ya kuwasimamisha viongozi walioingia madarakani
kikatiba, kwa kisingizio cha timu yao kushindwa kufanya vizuri kwenye
fainali za kombe la dunia zinazofikia tamati mwishoni mwa juma hili huko
nchini Brazil.
Kusimamishwa kwa NFF, kutaithiri nchi ya Nigeria katika ushiriki wa
michezo ya soka duniani kote, ambapo kuanzia usiku wa kuamkia hii leo
shughuli zote za mchezo huo nchini humo hazitovuka mipaka.
Hatua hiyo inaashiria wazi kwamba timu ya taifa ya wanawake ya
Nigeria chini ya umri wa miaka 20 ambayo ilistahili kushiriki mchuano wa
kombe la dunia iliyopangwa kufanyika nchini Canada kuanzia August 5–24
haitokwenda kushiriki.
Hata hivyo FIFA walikuwa wametoa muda wa viongozi wa serikali ya
nchini Nigeria kubatilisha maamuzi yao ifikapo siku ya jumanne, lakini
lakini Serikali ilipuuza maagizo hayo.
Mwishoni mwa juma lililopita serikali ya Nigeria ilimteuwa afisa wa
muda kwa ajili ya kuliongoza shirikisho la soka NFF hadi uchaguzi wa
huru na wa haki utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya
michezo.
0 comments:
Post a Comment