Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Mhe Hawa Ghasia leo ametumia zaidi ya milioni 90 kukabidhi vitu mbalimbali alivyokuwa ameahidi katika jimbo lake la mtwara Vijijini.
Miongoni mwa Vitu alivyokabidhi leo ni pamoja na bati 1700, Jezi seti 28 pamoja Pikipiki 28 na kusisitiza kuwa ataendelea kutimiza ahadi zake alizoahidi kwa wapiga kura wake wa Jimbo la Mtwara Vijijini
Aidha Mhe Ghasia amewataka wananchi wa Mtwara Vijijini kushirikiana katika kuleta maendeleo kwa wilaya yao kwa kuunda vikundi vya ujasiliamali ambavyo yeye anauwezo wa kuvisaidia kuliko kumsaidia mtu mmoja mmoja
Katika hauta nyingine Mhe ghasia amewataka wananchi hao kutumia vizuri vifaa hivyo walivyopewa na kuvitthamini zaidi
Kutimizwa kwa ahadi hizo za vitu mbalimbali alivyovito leo kumenyamazisha maneno ya viongozi wa upinzani waliokuwa wakibeza utendaji kazi wake mara kadhaa kupitia vikao vyao vya ndani vya vyama hivyo
Watu mbalimbali hawakujiuzia kutoa shukrani zao baada ya mhe Ghasia kutoa vitu hivyo...hiki ndicho alichoandika mwenyekiti wa Vijana mtwara Vijijini kutoka CCM Seleman Sankwa
Selemani Sankwa·HONGERA
SANA MH.HAWA GHASIA.UMETOA PIKIPIKI 28,MABATI 1700,JEZI SETI 28.HAKIKA
NI ZAIDI YA MILIONI 90 LEO UMETOA.MUNGU AKUBARIKI.JUHUDI ZAKO TUNAZIONA
NA TUNAZITHAMINI.

0 comments:
Post a Comment