Home » » Ridhiwani Kikwete Ashinda Chalinze kwa Asilimia 86

Ridhiwani Kikwete Ashinda Chalinze kwa Asilimia 86

 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushinda kiti hicho cha ubunge katika uchaguzi uliofanyika jana
 
Uchaguzi mdogo katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani, jana ulifanyika kwa utulivu na mgombea kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Ridhiwani Kikwete akiibuka kidedea baada ya kuwaburuza kwa mbali wagombea wenzake kutoka vyama vya upinzani.

Uchaguzi mdogo katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani, jana ulifanyika kwa utulivu na mgombea kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Ridhiwani Kikwete akiibuka kidedea baada ya kuwaburuza kwa mbali wagombea wenzake kutoka vyama vya upinzani.

Aidha uchanguzi huo ulishuhudia wapiga kura wachache wakijitokeza wengi wakiwa ni wazee.
Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete walipiga kura kijijini kwao Msoga katika shule ya msingi ya Msonga na Rais Kikwete kusema alifurahi kutimiza haki yake ya kikatiba ya kupiga kura na kwamba amemchagua mgombea wa CCM.

Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo Bw. Samweli Sariangi, alisema hali ilikuwa nzuri kwani hawakuwa wamepata malalamiko yoyote.

Ridhiwani Kikwete ameshinda kwa kura 28,828 ikiwa ni asilimia 86.6 ya kura zote zilizopigwa dhidi ya kura 2,544 sawa na asilimia 10.5 alizopata mgombea wa CHADEMA na kura 476 sawa na asilimia 1.9 alizopata mgombea wa CUF.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho mbunge mteule wa jimbo la Chalinze bwana Ridhiwan Kikwete amesema anawashukuru wanachalinze kwa imani yao kwake na chama chake na kuahidi kushirikiana nao kushughulikia changamoto za jimbo hilo huku mpinzani wake pekee aliyekuwepo kusikiliza matokeo bwana Husen Ramadhan wa NRA akikubali matokeo hayo.

Zoezi hilo la upigaji kura kumchagua mbunge wa jimbo la Chalinze lilifanyika hapo jana ambapo kati ya wapigakura zaidi ya elfu 92 walioandikishwa kwenye daftari la kudumu jimboni humo ni wapigakura 24,422 pekee waliojitokeza kupiga kura hali inayoacha changamoto kwa tume ya taifa ya uchaguzi kutafuta ufumbuzi wa suala la watu kutojitokeza kupiga kura.
 

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303