Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na rais wa Rwanda Paul Kagame(picha na maktaba yetu)
Serikali ya Tanzania imefafanua kuwa uhusiano kati
ya Tanzania na Rwanda ni mzuri na kwamba hali ni tofauti na ambavyo vyombo vya
habari vya nchi hizo vimekuwa vikiripoti katika kipindi cha miezi sita
iliyopita.
Waziri wa nchi, ofisi ya Rais asiyekuwa na wizara maalumu Profesa Mark Mwandosya, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ambapo watu laki nane waliuawa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Waziri Mwandosya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, amevitaka vyombo vya habari kuachana na kauli zenye uchochezi na zinazoweza kuvunja uhusiano baina ya nchi hizo, huku akizitaka mamlaka za serikali kudumisha mahusiano na nchi ya Rwanda ikiwa ni pamoja na usafiri wa kila siku kati ya Dar es Salaam na Kigali pamoja na ziara za kimafunzo kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
0 comments:
Post a Comment