Mshambuliaji anayetajwa kuondoka Yanga, Said
Bahanuzi, amezua hofu baada ya kutoonekana mazoezini kwa siku mbili mfululizo
huku benchi la ufundi likiwa halina taarifa zake.
Bahanuzi ambaye hivi karibuni amekuwa
akihusishwa kuwaniwa kwa karibu na Stand United ya Shinyanga, amekuwa na wakati
mgumu Jangwani mbele ya makocha watatu waliopita klabuni hapo huku akibaki kuwa
staa wa michuano ya Kagame ya mwaka 2012 ambapo aliibuka mfungaji bora.
Straika huyo hajaonekana mazoezini tangu juzi
Jumatano kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo na inaelezwa
kuwa benchi la ufundi halina taarifa zozote juu yake.
“Mhh..! kweli Bahanuzi
hayupo na hajaonekana mazoezini kwa siku mbili, sijajua yupo wapi,” alisema
mtoa habari wetu.
Taarifa
nyingine zilieleza alikuwa mgonjwa na aliomba ruhusa, upande mwingine
umeeleza yuko katika maandalizi ya kutua Stand United ya Shinyanga na
simu yake haikupatikana.
0 comments:
Post a Comment