Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA limesema mafuriko yameripotiwa
katika maeneo kadhaa nchini Somalia na kuathiri watu elfu 50.
Naibu msemaji wa
Umoja wa Mataifa Bw Farhan Haq amesema hata hivyo mashirika ya dharura yalikuwa
na misaada tayari kukabiliana na janga hilo.
Tangu mwezi Oktoba
mvua kubwa nchini Somalia imesababisha mafuriko katika mito ya Shabelle na
Juba.
0 comments:
Post a Comment