Home » » NIGERIA YAISHUTUMU MAREKANI KUHUSU VITA DHIDI YA BOKO HARAM

NIGERIA YAISHUTUMU MAREKANI KUHUSU VITA DHIDI YA BOKO HARAM



Balozi wa Nigeria nchini Marekani Ade Adefuye ameishutumu Marekani kuwa haijatoa usaidizi wa kutosha katika vita dhidi ya kundi la waasi la Boko Haram.
Adefuye amedai Marekani imeshindwa kuipa Nigeria taarifa za kijasusi na kuiuzia silaha zinazohitajika kupambana na kundi hilo linaloendeleza uasi kaskazini mwa Nigeria.
Katika maoni yaliyochapishwa katika mtandao wa ubalozi wa Nigeria nchini Marekani,balozi huyo ameitaka Marekani kuiunga mkono kikamilifu nchi yake na kukanusha madai kuwa kuna ukiukaji wa haki za binadamu upande wa serikali ya Nigeria unaoizuia Marekani kutoa msaada wa kijeshi.
Afisa wa utawala wa Rais wa Marekani Barrack Obama akijibu shutuma hizo, amesema Marekani inasalia kujitolea kuisaidia Nigeria kukabiliana na kitisho cha waasi wa Boko Haram na inaendelea na juhudi za kusaidia kuokolewa kwa mateka wanaozuiwa na waasi hao.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ambaye ametangaza kuwania muhula wa pili ameshutumiwa vikali kwa kushindwa kukabiliana vilivyo na Boko Haram.

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303