Home » » NDANDA KUONGEZA SITA DIRISHA DOGO

NDANDA KUONGEZA SITA DIRISHA DOGO

Uongozi wa timu ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara, upo katika harakati za kusajili wachezaji sita kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara.
 
Timu hiyo ambayo ilipanda ligi kuu msimu uliopita, imeonekana kusuasua katika ligi hiyo kwa kucheza michezo saba na kufanikiwa kushinda miwili huku ikifungwa mitano na sasa ipo katika nafasi ya 13 baada ya kujikusanyia pointi sita kwenye msimamo wa ligi.
 
Kocha wa timu hiyo, Abdul Mingange, alisema ameshakabidhi ripoti yake kwa uongozi wa timu hiyo baada ya kucheza michezo miwili kufuatia kutimuliwa kwa kocha aliyeipandisha ligi kuu, Dennis Kitambi ili kuipitia na kuona upungufu uliopo.
 
Alisema nafasi zinazotakiwa kufanyiwa usajili kwa timu hiyo ni kipa, beki, kiungo mkabaji, kiungo mshambuliaji na mshambuliaji kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ili kuweza kufanya vizuri katika michezo inayofuata.

“Tunatarajia kufanya usajili wa wachezaji sita ili kuweza kuimarisha nguvu kwenye kikosi ili kuziba upungufu uliopo na kupigania ushindi kwenye ligi kwa ajili ya kushika nafasi za juu,” alisema Mingange ambaye ni meja mstaafu wa Jeshi la Wananchi.

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303