Timu ya Soka ya Ndanda ya Mkoani Mtwara imeingia Kambini Jana kujiandaa na Michezo ya ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kurejea tena Oktoba 17 Mwaka huu Baada ya kusimama kwa Wiki mbili kupisha Mchezo wa Kimataifa wa Taifa Stars dhidi ya Malawi Jumatano hii.
Akithibitisha kuingia kambini kwa Timu hiyo Afisa Habari wa Ndanda Fc Idrisa Bandali amesema, Kambi yao wameweka huko Ndanda kwenyewe ili kuwapa Wachezaji nafasi kubwa ya kujiandaa ili kufanya Vizuri kwenye Michezo yao ijayo
"tunataka kuwapa muda mrefu zaidi walimu wetu wa kuhakikisha wanatoa dozi nzuri kwa wachezaji wetu na wapate muda wa kupumzika kama unavyojua huku ni kijijini sio mjini kwa hiyo wachezaji watakuwa na muda mrefu wa kufikiria mpira zaidi"
Ndanda Fc imecheza Michezo Mitano imeshinda Mchezo mmoja, imetoka sare michezo miliwi na imepoteza michezo miwili hivyo kujikusanyia Pointi 5 na wako nafasi ya 11 kwenye Msimamo wa Ligi kuu kama unavyoonyesha hapa chini.
0 comments:
Post a Comment