Timu ya Waandishi wa habari Mkoani Mtwara imejinasibu
kuibuka na Ushindi dhidi ya Timu ya Jukwaa la Wahariri mechi itakayochezwa
Jumamosi hii Mkoani Mtwara
Akizungumza na BANDALI 44 Mwenyekiti wa Chama cha Waaandishi wa
Habari
Mkoani Mtwara Bw Hassani Simba amesema wako katika maandalizi makali
kwani wanatambua Timu wanayokutana nayo ni Nzuri hivyo hawana budi kufanya
mazoezi ya Nguvu ili kutoa upinzani wa hali ya juu siku hiyo
Simba amesema…unajua wenzetu hawa timu yao ni nzuri
na utakumbuka wiki chache zilizopita walikuwa Iringa na wamewafunga waandishi
wa Iringa goli 4-0 kwa hiyo na sisi ili kukwepa aibu ya kufungwa lazima tufanye
mazoezi ya nguvu ili kujiweka sawa na lazima tuibuke na ushindi hiyo siku…alisema
Simba
Aidha Simba ameongeza kuwa Uwanja unaotumika kwa
mazoezi yao na ambao pia utatumika kwa ajili ya Mchezo huo ni uwanja wa Chuo
cha Uwalimu Mtwara (TTTC) na kuwaomba waandishi wote kuhudhulia mazoezi
yanayoanza rasmi leo
Kuhusu Vifaa Simba amesema…Leo Julai 9 tunatarajia
kupewa Jezi na Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe Hasnein Murji ili kutoa motisha kwetu
kwa ajili ya mechi hiyo kubwa , kwa hiyo tutaingia na uzi mpya na ni mbaya
ukiingia na uzi mpya halafu ukafungwa kwa hiyo lazima tushinde
Simba amewataja wachezaji wanaotegemewa kukiongoza
Kikosi cha Mtwara Press Club kuwa Ni pamoja na Mtuli Kutoka Pride Fm, Marino
Kawishe Kutoka Safari Radio, Brayson Mshana Kutoka southern Media Solution ,
Rajabu Lukanga Kutoka Info Radio, Idrisa Bandali kutoka Newala fm, Modestus
Mwambe,Fakihi Mussa , Filipo Lulale na wengine wengi
0 comments:
Post a Comment