Home » » UNAIJUA ADHABU ALIYOIPATA SUAREZ? IKO HAPA ISOME

UNAIJUA ADHABU ALIYOIPATA SUAREZ? IKO HAPA ISOME


CHIELLINI-MENOSUAREZ_AUMA_TENA2
STRAIKA wa Uruguay Luis Suarez amefungiwa Miezi Minne kutoshiriki chochote kwenye Soka baada ya kupatikana hatia ya kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini.

Straika huyo wa Liverpool pia amefungiwa Mechi 9 za Kimataifa zitakazomfanya awe nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.

Adhabu hii pia inamaanisha atazikosa Mechi 9 za kwanza za Klabu yake Liverpool za Ligi Kuu England kwa Msimu mpya.

Tukio hili la kumng’ata Meno Chiellini lilitokea Juzi Jumanne kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia ambayo Uruguay iliifunga Italy 1-0 na kutinga Raundi ya Pili ya Mtoano.

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303