Home »
Michezo
» SIMBA SC YAWAALIKA WANACHAMA, WANAHABARI KUONA MAENDELEO YA UWANJA BUNJU
Azam fc pekee ndio klabu ya Tanzania
yenye uwanja wake wa kisasa kwa ajili ya mazoezi, mechi za ligi kuu na michuano
yote inayosimamiwa na shirikisho la soka barani Afrika, CAF.
Katika historia ya soka la Tanzania,
Azam fc haiwezi kunusa ukongwe wa klabu mbili za Simba na Yanga.
Hizi ni klabu zenye mafanikio ndani
na nje ya uwanja. Ni klabu zenye mashabiki kila kona ya nchi hii.
Lakini licha ya kukaa miaka mingi
katika soka la ushindani nchini Tanzania na michuano ya Kimataifa, Yanga na
Simba hazijawahi kumiliki viwanja vyake vya mazoezi na mechi za ligi kuu.
Kwa miaka mingi sasa viongozi
wanaopita katika klabu hizo wanakuja na ndoto za kujenga viwanja, lakini
zinayeyuka kutokana sababu mbalimbali ikiwemo kuendekeza siasa kuliko vitendo.
Kwasasa mwenyekiti wa Yanga, Yusuf
Manji ana mkakati kabambe wa kujenga uwanja wa klabu hiyo maeneo ya Jangwani,
wakati huo huo, naye mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Rage akipambana na
mpango kama huo maeneo ya Bunju jijini Dar es salaam.
Kwa miezi miwili sasa, Uongozi wa
Simba unaendelea na ujenzi wa uwanjao wake na sasa umefikia hatua nzuri ya
kuanza kutumika kwenye mazoezi ya klabu hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kumiliki
uwanja katika historia yake.
Kutokana na maendeleo hayo,uongozi
wa Simba umewakaribisha wapenzi na wanachama wake kesho Jumamosi katika Uwanja wao Bunju kwa ajili ya
kuangalia maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu.
Katibu mkuu wa Simba sc, Ezekiel
Kamwaga amesema ujenzi huo ulioanza miezi miwili iliyopita, unakaribia
kukamilika na utakuwa uwanja wa kwanza rasmi wa mazoezi wa klabu katika
historia yake.
Vyombo vya habari navyo vinaalikwa
katika tukio hilo litakaloanza saa tano kamili asubuhi.
0 comments:
Post a Comment