Barabara ya Arusha-Holili upande wa Tanzania pia
inakarabatiwa.
Rais Kikwete yumo nchini Kenya kwa ziara rasmi ya
siku tatu na Jumanne anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha mabunge mawili
ya Kenya.
Mradi wa ujenzi wa barabara hizo mbili
umefadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali za Kenya na
Tanzania.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kanda hii wa AfDB
Gabriel Negatu benki hiyo imetoa $218 milioni za kutumiwa kwenye mradi huo,
Kenya ikipokea $116 milioni na Tanzania $102 milioni.
Huo ndio mradi wa pili wa barabara wa kuunganisha
Kenya na Tanzania uliofadhiliwa na benki hiyo, wa kwanza ukiwa barabara za
Arusha-Namanga/Namanga-Athi River.
Rais Kikwete alisema barabara hiyo ya
Taveta-Mwatate hutumiwa na wakazi wa kaskazini na kaskazini-magharibi mwa
Tanzania kusafirisha bidhaa hadi Mombasa.
“Huchukua saa 14 kutoka Arusha hadi Voi. Lakini
ujenzi huu ukikamilika, itachukua saa mbili na nusu pekee, hivyo kuwa nafuu
sana kwa wasafiri na wenye magari,” alisema.
Kiongozi huyo, anayetarajiwa kuondoka mamlakani
karibuni baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, alisema barabara hiyo ina uwezo wa
kuimarisha biashara kati ya Kenya na Tanzania kwa asilimia 10.
0 comments:
Post a Comment