Kiungo Andrey Coutinho, amerejea nchini jana tayari kuanza kazi na kikosi chake cha Yanga.
Mwenzake,
Geilson Santana 'Jaja' ameamua kubaki kwao Brazil na nafasi yake
imechukuliwa na kiungo Emerson Roque aliyetua jana pia.
Coutinho
amesema anaamini ameajiandaa vizuri na ataongeza mazoezi zaidi akiwa na
wenzake, pia ana hamu kubwa ya kuonyesha mabadiliko.
"Kweli
nimefanya sana mazoezi, lakini bado nahitaji kuungana na wenzangu na
kuendelea kujifua zaidi," alisema Coutinho akionyesha kufurahia kurejea
nchini.
0 comments:
Post a Comment