Home » » BAADA NYA KUWASILISHWA KWA RIPOTI YA ESCROW JANA, HAYA NI MAJIBU YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUHUSU KUJIUZURU

BAADA NYA KUWASILISHWA KWA RIPOTI YA ESCROW JANA, HAYA NI MAJIBU YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUHUSU KUJIUZURU

Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ua Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

“…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen, tumeiona Serikali ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’ ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata vilema…“– Mbowe.
Tumeona mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko curent sasa hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
Baada ya Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali nini msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio fedha za umma?“– Mbowe.
Kwa uzito huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsiu na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka kutaka litokee hilo lakini mambo haya yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…“
Ningeweza nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya kufanya hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa Bungeni ambao unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na mimi nitapata nafasi ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa yote Bunge litakuwa limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa uhakika ni hatua stahiki namna gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA NASI | 0783 561 514

 
Idrisa Bandali Available On : Facebook | Instagram | Twitter
Copyright © 2013. BANDALI 44 -Haki Zote Zimehifadhiwa
Blog Hii Imetengenezwa Na Ernest James Siwigo Inamilikiwa Na Idrisa Bandali
2brothers Inc 0719766915 | 0764214303