Mshambulizi wa Ujerumani Miroslav Klose ameweka rekodi ya kuwa mfungaji wa magoli mengi zaidi katika historia ya kombe la dunia.
Klose ndiye aliyefunga bao la pili Ujerumani iliposhinda bao 7 – 1
dhidi ya Brazil katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia
huko Belo Horizonte.
Klose mwenye umri wa miaka 36 mpaka sasa amefunga jumla ya mabao 16
baada ya kushiriki michuano minne ya kombe la dunia.
Aliyekuwa
akishikilia rekodi hio ni Ronaldo wa Brazil. Klose amefunga mabao 16.
Rekodi ya awali ya Ujerumani ilikuwa inashikiliwa na Gerd Mueller
Kufuatia Ushindi huo Ujerumani imefuzu kwa fainali yake ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi na miwili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment