Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Newala Mheshimiwa Rashidi Ndembo na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Newala Ndugu Marx Kamaoni wamewaasa wananchi wa wilaya
ya Newala kujitolea kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo inapoletwa katika
vijiji vyao.
Mheshimiwa
Ndembo na Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Kamaoni waliyasema hayo
wakati wa ziara ya Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ilipotembelea
miradi ya wilaya ya Newala jana.
Kamati
ya Fedha na Mipango ilipokuwa ikitembelea miradi ya halmashauri, miradi mingi
ilionekana kutomalizika kutokana na fedha kutotosheleza kumalizia miradi hiyo.
Hii imetokana na fedha inayotolewa na serikali kutumika katika shughuli zote za ujenzi
kuanzia usombaji maji, michanga na mawe, kazi ambayo ingeweza kufanywa na
wananchi wa kijiji husika na fedha kutumika katika ununuzi wa vifaa vya
viwandani kama mabati, mbao na simenti.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri aliwaambia baadhi ya wanavijiji waliojitokeza wakati wa
ukaguzi wa miradi hiyo kujitolea katika ujenzi wa miradi ya maendeleo aliwaambia kuwa serikali inapotoa fedha kwa ajili ya ujenzi
wa miradi wananchi nao wanatakiwa kuchangia ili fedha inayotolewa na serikali
iweze kununulia vifaa vya viwandani ili kuboresha miradi hiyo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri aliwaambia wananchi kuwa, kijiji chochote kitakachooneka
kutoshiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo basi miradi itahamishiwa
kijiji kingine ambacho wananchi wake wako tayari kujitolea kushiriki ujenzi wa
miradi ya maendeleo.
Miradi
iliyotembelewa na Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ni Mradi wa ujenzi wa
nyumba ya mtumishi na wodi ya Mkwedu, ujenzi wa nyumba ya mwalimu Chitenda, ujenzi
wa nyumba ya mwalimu Mkoma II, ujenzi wa nyumba ya mwalimu Chilende, ujenzi wa
nyumba ya mwalimu Mchemo, ujenzi wa nyumba ya mwalimu Mmulunga, ujenzi wa mradi
wa maji Mmulunga na mashine ya kukamulia Alizeti Idamnole – Chihangu.
Mwenyekiti
wa halmashauri na Mkurugenzi wa halmashauri waliambatana na madiwani wengine
saba pamoja na wataalamu ambao wanaunda kamati ya Fedha, utawala na Mipango ya halmashauri.
0 comments:
Post a Comment