BAADA ya mvutano kuhusu aina ya kura itakayotumika kupitisha vifungu
vya rasimu ya Katiba, hatimaye Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba,
Samuel Sitta ametangaza kutumika kwa njia ya maridhiano kumaliza utata.
Mvutano huo ni kuhusu ama kupigwa kura ya wazi au ya siri, jambo
ambalo ililazimika uamuzi juu ya suala hilo, uwekwe kiporo wakati wa
kupitisha kanuni.
Sitta alisema majadiliano hayo, yenye lengo la kufikia maridhiano,
yatafanyika kupitia makundi mbalimbali yanayounda Bunge hilo kufikia
mwafaka kuhusu utaratibu, utakaotumika kupitisha vifungu namba 37 na 38
vya kanuni za Bunge hilo.
Sitta aliliambia Bunge makundi hayo, yataanza mjadala wa maridhiano
leo baada ya kupatikana kwa wenyeviti wa kamati 12 za Bunge hilo.
Licha ya suala hilo kutegemea kupatikana wenyeviti, vile vile
linategemea kupatikana kwa Kamati ya Uongozi ya Bunge inayoundwa na
wenyeviti wa kamati zote.
Mwenyekiti anaruhusiwa pia kikanuni, kuongeza wajumbe watano kuleta uwiano mzuri wa Kamati hiyo ya Uongozi.
Alisema baada ya majadiliano baina ya makundi hayo kukamilika, uamuzi
utafikiwa juu ya kupitisha vifungu hivyo kwa mujibu wa kanuni, hatua
itakayofanya kukamilishwa kwa uandaaji wa kanuni zote za Bunge hilo.
Uchaguzi wa wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati ulifanyika jana.
Zikiachwa kamati 12 za Bunge hilo, nyingine ni za kitaalamu ambazo ni
Kamati ya Uandishi na Kamati ya Kanuni na Haki.
Kwa mujibu wa Sitta, Bunge hilo pia litaboresha baadhi ya vifungu vya
kanuni kuzipa uwezo na utaratibu mzuri zaidi wa uendeshaji wa Bunge
hilo, ikiwemo kuweka utaratibu wa kikanuni wa kufanya uamuzi kwenye
Kamati kutokana na kanuni ya 38 kifungu kidogo cha pili, kutoeleza jinsi
ya kufanya uamuzi kwenye Kamati.
Alisema uboreshaji mwingine utakuwa ni juu ya namna ya kuongoza
majadiliano kwenye Kamati, ambapo Kamati ya Uongozi itakayoundwa
itashauriana na baadaye kuwasilisha mapendekezo ya uboreshaji huo kwa
Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge ili iwasilishe Azimio la marekebisho
hayo katika Bunge zima kupitisha au vinginevyo.
Kamati zaundwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta,
ameunda kamati 12 zitakazojadili ibara za rasimu ya Katiba mpya na
kuleta mapendekezo yao katika Bunge Maalumu kwa ajili ya kujadiliwa na
kupitishwa.
Mbali na kamati hizo 12, Mwenyekiti huyo pia ameunda kamati zingine
mbili, moja ya Uandishi wa Katiba na nyingine ya Kanuni na Haki za Bunge
Maalumu.
Mwenyekiti huyo pia, anatarajiwa kuunda Kamati ya Uongozi wa Bunge
Maalumu baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa wenyeviti na makamu
wenyeviti wa kamati 12 za kujadili ibara za Rasimu ya Katiba mpya.
Akitangaza kamati hizo bungeni jana, Sitta alisema katika uundaji wa
kamati hizo ambazo zitapewa majukumu ya kujadili ibara zaidi ya mbili
kila moja, alizingatia uwiano wa vigezo mbalimbali walivyonavyo wajumbe
wa Bunge Maalumu.
Kigezo cha kwanza alizingatia idadi, ambapo kamati zote zina wajumbe
52 isipokuwa Kamati namba moja, yenye wajumbe 53. Kila kamati pia
ilipata wajumbe wa jinsi zote na kutoka kila upande wa Muungano.
Aidha, kila kamati imepata wajumbe kutoka Bunge la Jamhuri ya
Muungano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kundi la wajumbe wa
kuteuliwa ambapo jana jioni kila moja ilitakiwa kukutana katika kumbi 12
nje ya Bunge, kuchagua Mwenyekiti wa Kamati na Makamu Mwenyekiti.
|

0 comments:
Post a Comment