Huduma za usafiri jijini Nairobi zimekwama kufuatia
hatua za wenye magari kugoma hii leo wakilalamikia nyongeza ya ada ya
kuegesha magarji jijini humo.
Maelfu ya wafanyakazi wamelazimika kutembea kwa
miguu na wasafiri wa kutoka jijini kwenda maeneo ya mashambani nao
kulazimika kuahirisha safari zao.
Mwenyekiti
wa wenye matatu katika eneo la Mlima Kenya, Bwana Michael Kariuki,
ambaye aliongea na BBC akiwa nje ya lango la kuingia kwenye afisi ya
Gavana wa Kaunti ya Nairobi, alisema mzozo uliopo ni mdogo na waweza
kusuluhishwa haraka.
"Juzi tulikuwa na Gavana Evans Kidero na
tukakubaliana kiasi tunachopaswa kulipa lakini jana tulipofika
wafanyakazi wa kaunti wakakataa kiasi tulichokuwa nacho," Bwana Kariuki
alisema.
Jiji la Nairobi ni mojawapo wa kaunti ambazo
zimebuniwa chini ya Katiba iliyopitishwa na wapiga kura na kuidhinishwa
mwaka 2010 katika hatua ya kuimarisha huduma kwa wananchi.
Kaunti hizo mpya hata hivyo zimejikuta njia
panda baada ya kupata madaraka bila fedha za kuandamana nayo; ambapo
zimelazimika kuongeza kodi kama njia mojawapo ya kujiimarisha kiuchumi.
|
MAGARI YA UMMA YAVURUGA SHUGHULI NAIROBI
Imetumwa Na Unknown
Posted on 2:58 AM
with No comments
0 comments:
Post a Comment