Picha kwa hisani ya Mwananchi |
HABARI TULIZONAZO
Wabuge wa Upinzani Leo wametoka Nje kwa aina nyingine ya Mgomo kwa kuziba Midomo yao na Plasta
Imetumwa Na Unknown
Posted on 1:53 AM
with No comments
UMEIONA REKODI YA AZAM FC DHIDI YA COASTAL UNIONI, IKO HAPA NIMEKUWEKEA
Imetumwa Na Unknown
Posted on 9:10 PM
with No comments
KLABU
Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC ina rekodi ya asilimia 100 ya
kutopoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Coastal
Union.
Azam
FC inatarajia kumenyana na Coastal Union Jumapili hii (Februari 14) katika
mchezo wa ligi utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwa
mujibu wa takwimu za ligi hiyo tokea Azam FC ianze kucheza Ligi Kuu msimu wa
2008/2009, zinaonyesha kuwa imekutana mara tisa na Coastal Union kwenye mechi
za ligi, ikishinda mara saba na kutoka sare mbili.
Katika
mechi hizo, zilizochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani ni nne pekee, ambapo Azam
FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB imeshinda mbili (1-0, 1-0) na nyingine mbili
zikiisha kwa sare (0-0, 1-1), huku Azam FC ikishinda mechi tano zote
zilizochezwa Azam Complex.
Jumla
ya mabao 21 yamefungwa kwenye mechi hizo zote tisa, ambapo Azam FC imefunga
asilimia 98 ya mabao yote ikitupia 18 na Coastal ikifunga matatu pekee.
Azam
FC pia Julai mwaka jana ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal Union
pamoja na African Sports kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame, na
ikawachapa Wagosi wa Kaya hao bao 1-0, lililofungwa na Ame Ally.
Kuelekea
mchezo wa Jumapili hii, tayari Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, ameweka
wazi kuwa anataka kuendeleza rekodi waliyoweka ya kufanya vizuri kwenye mechi
za ugenini msimu huu pamoja na ile waliyonayo ya kufanya vema katika Uwanja wa
Mkwakwani.
Azam
FC ambayo ni miongoni mwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo, mpaka sasa ndio timu
pekee iliyokuwa na rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi katika mechi 16
walizocheza, ikishinda 13 na sare tatu ikijikusanyia jumla ya pointi 42 sawa na
Simba iliyo nafasi ya pili huku ikizidiwa pointi moja tu na Yanga inayoongoza
ligi kwa pointi 43.
Lakini
matajiri hao wa Azam Complex wana mechi mbili mkononi, zinazoweza kuwaweka juu
kileleni kwa tofauti ya pointi tano kwa atakayemfuatia kama ikizishinda zote.
REKODI
AZAM FC V COASTAL UNION
2011/2012
Coastal
Union 0-1 Azam FC (Septemba 21, 2011)
Azam
FC 3-0 Coastal Union (Machi 07, 2012)
2012/2013
Azam
FC 4-1 Coastal Union (Novemba 01, 2012)
Coastal
Union 1-1 Azam FC (Aprili 26, 2013)
2013/2014
Coastal
Union 0-0 Azam FC (Oktoba 05, 2013)
Azam
FC 4-0 Coastal Union (Machi 15, 2014)
2014/2015
Azam
FC 2-1 Coastal Union (Novemba 08, 2014)
Coastal
Union 0-1 Azam FC (Machi 22, 2015)
2015/2016
Azam
FC 2-0 Coastal Union (Septemba 30, 2015)
Coastal
Union ?-? Azam FC (Februari 14, 2016)
AIR TANZANIA YAISAFIRISHA YANGA KUELEKEA MAURITIUS
Imetumwa Na Unknown
Posted on 9:05 PM
with No comments
Yanga
inaondoka kesho saa 11 Alfajiri kwenda Mauritius katika mechi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim SC.
Kikosi cha
Yanga kinaondoka na ndege ya kukodi ya kampuni ya Air Tanzania na itatumia saa
nne na ushee angani ikiwa njiani kwenda nchini humo.
Ikiwa
nchini humo, ndege hiyo itakuwa imepaki pembeni ikiisubiri Yanga ikiwa
mazoezini, ikiwa hotelini hadi siku ya mechi.
Yanga
inatarajia kushuka dimbani ikiwa ugenini na itatakiwa kushinda au kufanya
vizuri kabla ya mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam.
Baada ya
mechi hiyo, ndege hiyo itaruka hadi Pemba moja kwa moja kuepuka kupitia jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya kambi.
MKWASA KIBARUANI KUWAAMINISHA WATANZANIA, STARS KUWAFUTA MACHOZI WAPENDA SOKA
Imetumwa Na Unknown
Posted on 2:16 AM
with No comments
Tanzania leo wanaikaribisha Malawi katika mchezo wa kwanza wa
kuwania kupangwa kwenye makundi ya kugombea tiketi ya kucheza Fainali za Kombe
la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Taifa Stars inakutana na Malawi leo, ikitoka kucheza mechi 11 bila kushinda. Mara ya mwisho Taifa Stars ilishinda 4-1 dhidi ya Benin Oktoba 12, mwaka jana Dar es Salaam na tangu hapo imekuwa ikichezea vichapo mfulilizo na kutoa sare.
Stars inacheza na Malawi siku moja baada ya kocha Mzalendo, Charles Boniface Mkwasa kusaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu, akirithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amesema jana kwamba Mkwasa amesaini Mkataba wa kudumu Taifa Stars, sawa na wa
mtangulizi wake, Mholanzi Mart Nooij.

Malinzi alimteua Mkwasa kukaimu Ukocha Mkuu Taifa Stars kwa miezi mitatu tangu Julai na akasema kwa kuanzia atakuwa anachukua mshahara alikuwa analipwa Nooij.
Nooij aliyekuwa analipwa dola za Kimarekani 12,500 (zaidi ya Sh. Milioni 25) kwa mwezi, alifukuzwa mwishoni mwa Juni baada ya Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Uganda Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mechi ya kufuzu CHAN.
Mkwasa aliwateua Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ kuwa Mshauri wa Ufundi, Hemed Morocco kuwa Kocha Msaidizi na Manyika Peter kuwa kocha wa makipa wakichukua nafasi za Salum Mayanga na Patrick Mwangata.
Aidha, Omar Kapilima aliteuliwa kuwa Meneja na Hussein Swedi ‘Gaga’ kuwa mtunza vifaa vya timu- kukamilisha sura mpya kabisa ya benchi la Ufundi la Taifa Stars.
Na tangu hapo timu imecheza mechi tatu bila ushindi ikitoa
sare ya 1-1 na Uganda mjini Kampala kufuzu CHAN, ikifungwa 2-1 na Libya mchezo
wa kirafiki mjini Kartepe, Uturuki na kutoa sare ya 0-0 na Nigeria.
Hayo yalikuwa mabadiliko makubwa kutoka kwenye timu kufungwa mechi tano mfululizo na kwa ujumla kucheza mechi 11 bila ushindi chini ya Nooij.
Taifa Stars watasafiri Ijumaa asubuhi kwenda Malawi kurudiana nao Jumapili mjini Blantyire na mshindi wa jumla ataingia kwenye Raundi ya pili ya kufuzu ambako atamenyana na Algeria.
Atakayefuzu mtihani wa Algeria, atakuwa amefanikiwa kupangwa kwenye Kundi la kuwania tiketi ya kwenda Urusi mwaka 2018.
Wachezaji wote wanaocheza nje, Mrisho Ngassa wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC wapo kambini.
Watatu hao wamekuja wakiwa katika kiwango kizuri, Ngassa akitoka kuisaidia klabu yake kufuzu Robo Fainali ya Kombe la Telkom Knockout na akina Samata na Ulimwengi wakitoka kuisaidia Mazembe kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kila la heri Taifa Stars. Mungu ibariki Tanzania. Amin.
Malinzi alimteua
Mkwasa kukaimu Ukocha Mkuu Taifa Stars kwa miezi mitatu tangu Julai na akasema
kwa kuanzia atakuwa anachukua mshahara alikuwa analipwa Nooij.

NDANDA YAENDELEA KUJIFUA LICHA YA KUWA NA MAJERUHI
Imetumwa Na Unknown
Posted on 2:09 AM
with No comments
Timu ya Soka ya Ndanda imeendelea na Mazoezi yake ikiwa Kambini huko Kijijini kwao Ndanda ambako Timu hiyo ndiko ilikoanzishwa Miaka 5 iliyopita.
Kocha Mkuu wa Ndanda Fc Hamimu Mawazo amesema Kikosi Chake Kiko Vizuri na kinaendelea na Mazoezi Licha ya kukumbwa na Majeruhi Kadhaa ambao wanaendelea na Matibabu
Mawazo amewataja Majeruhi hao kuwa ni Masoud Ally aliyeumia Goti kwenye Mchezo wao dhidi ya African Sport uliochezwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga na Ndanda kufungwa Moja kwa Sifuri, Mwingine ni Omari Mponda anayesumbuliwa na Kiuno.
Ndanda imeamua kuweka kambi yake Huko Ndanda ili kuweza kujiwinda na Michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara ukianzia na Ule wa Toto Afrika ya Mwanza Mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara
Kocha Mkuu wa Ndanda Hamimu Mawazo Akizungumza na Waandishi wa Habari |
Mawazo amewataja Majeruhi hao kuwa ni Masoud Ally aliyeumia Goti kwenye Mchezo wao dhidi ya African Sport uliochezwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga na Ndanda kufungwa Moja kwa Sifuri, Mwingine ni Omari Mponda anayesumbuliwa na Kiuno.
Ndanda imeamua kuweka kambi yake Huko Ndanda ili kuweza kujiwinda na Michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara ukianzia na Ule wa Toto Afrika ya Mwanza Mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara
KIKWETE NA KENYATTA WAZINDUA BARABARA MUHIMU KENYA
Imetumwa Na Unknown
Posted on 4:42 AM
with No comments
Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta na mwenzake wa Tanzania Jakaya Kikwete wamezindua mradi wa ujenzi wa
barabara ya Taveta-Mwatate ambayo inatarajiwa kurahisisha uchukuzi kati ya
kataifa hayo mawili.
Barabara ya Arusha-Holili upande wa Tanzania pia
inakarabatiwa.
Rais Kikwete yumo nchini Kenya kwa ziara rasmi ya
siku tatu na Jumanne anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha mabunge mawili
ya Kenya.
Mradi wa ujenzi wa barabara hizo mbili
umefadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali za Kenya na
Tanzania.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kanda hii wa AfDB
Gabriel Negatu benki hiyo imetoa $218 milioni za kutumiwa kwenye mradi huo,
Kenya ikipokea $116 milioni na Tanzania $102 milioni.
Huo ndio mradi wa pili wa barabara wa kuunganisha
Kenya na Tanzania uliofadhiliwa na benki hiyo, wa kwanza ukiwa barabara za
Arusha-Namanga/Namanga-Athi River.
Rais Kikwete alisema barabara hiyo ya
Taveta-Mwatate hutumiwa na wakazi wa kaskazini na kaskazini-magharibi mwa
Tanzania kusafirisha bidhaa hadi Mombasa.
“Huchukua saa 14 kutoka Arusha hadi Voi. Lakini
ujenzi huu ukikamilika, itachukua saa mbili na nusu pekee, hivyo kuwa nafuu
sana kwa wasafiri na wenye magari,” alisema.
Kiongozi huyo, anayetarajiwa kuondoka mamlakani
karibuni baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, alisema barabara hiyo ina uwezo wa
kuimarisha biashara kati ya Kenya na Tanzania kwa asilimia 10.
KIINGILIO CHA CHINI STARS VS MALAWI TSH 5000
Imetumwa Na Unknown
Posted on 4:08 AM
with No comments
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Jumatano kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Malawi (The Flames) kuwa ni shilingi elfu tano (5,000) katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Viingilio vilivyotangazwa leo ni kiingilio cha juu kabisa kwa mchezo huo shilingi elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C, huku viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani ikiwa ni shilingi elfu tano (5,000).
Stars inayonolewa na kocha mzawa Charles Boniface Mkwasa imeendelea kujifua katika viwanja vya Gymkhana na uwanja Taifa jioni kujiandaa mchezo huo wa Jumatano dhidi ya Malawi, huku wachezaji wakiwa wenye ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mechi hiyo.
Wachezaji 22 wapo kambini akiwemo mshambuliaji Mrisho Ngasa anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini aliyeripoti jana mchana kambini, huku wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wakitarajiwa kujiunga na wenzao leo wakitokea Lubumbashi – Congo DR.
Wakati huo huo timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) imewasili nchini jana saa 4 asubuhi na kufikia katika hoteli ya De Mag iliyopo Mwanayamala, ambapo kikosi hicho leo kimefanya mazoezi asubuhi katika uwanja wa Boko Veterani.
Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Somalia, kamisaa na mtathimin waamuzi wa wanatarajiwa kuwasili leo nchini na kufikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.
Mwamuzi wa kati ni Hagi Yabarow Wiish (Somalia), akisaidiwa na Hamza Hagi Abdi (Somalia), Salah Omar Abubakar (Somalia), mwamuzi wa akiba Bashir Olad Arab (Somalia), mtathimini wa waamuzi Sam Essam Islam (Misri) na kamisaa wa mchezo ni Muzambi Gladmore (Zimbabwe).